CCI kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Ardhi, University College London na Shirikisho la Wakazi wa Maeneo Duni Tanzania (TUPF) waliongoza mjadala na wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi kuhusu changamoto za usafi wa mazingira katika Jiji la Mwanza.

Majadiliano hayo yalichambua mapungufu na mianya iliyopo kwenye kanuni ndogo zinazohusiana na shughuli za wafanyakazi wa usafi wa mazingira ambao ni pamoja na Frogmen (Vyura), Community Health Workers, wasafishaji (janitors na janitress) pamoja na wafanyakazi wengine wa vyoo vya umma.