Habari njema kwa wadau wote wa hali ya hewa. DARAJA App iliyotengenezwa na shirika la CCI kwa kushirikiana na UNDP na wadau wote wa maswala ya hali ya hewa sasa inapatikana Google Play store. Utaweza kupakua na kujisajili ili kupata taarifa za hali ya hewa. Pia unaweza ingia kama mgeni au kujisajili kama muuzaji au mnunuzi wa bidhaa mbalimbali ili usiishie tu kupata taarifa za hali ya hewa ila uone bidhaa za masoko za wakulima, wavuvi nk kwa Tanzania, hali ya foleni eneo lolote ulipo duniani na uhondo kemukemu. Link ya kupata DARAJA App kwa watumiaji wa Adroid ni hii: https://play.google.com/store/apps/details?id=com.daraja.app.weather_app_tutorial  au ingia mwenyewe Google Play Store upakue App yako. Kwa watumiaji wa Iphone bado App inaendelea kufanyiwa mchakato ili ipatikane pia App store. Maboresho zaidi yanakuja kwa kuweza kuunga taarifa za DARAJA kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) moja kwa moja kwenye App na tunakuomba upakue, utumie na utoe mapendekezo yeyote ili kuiboresha App yetu. Tunapenda kutambua mchango wa TMA na shirika la Resurgence katika kufanikisha hili. #MiminaHaliyaHewa# #IjueHaliyaHewaChukuaHatua#